"Karibu kwenye Scosiah E-Card – njia rahisi, ya kisasa na ya kuvutia ya kusherehekea tukio lako. Chagua muundo unaokufaa, tuma kwa wageni wako, na ufanye kila tukio kuwa la kukumbukwa."
Mteja anapewa sampuli kadhaa za Scosiah E-Card, kila moja ikiwa na muundo wa kisasa na rangi zinazovutia. Mteja anachagua muundo mmoja unaomfaa tukio lake.
Baada ya mteja kuchagua muundo, timu yetu inaendelea kufanya customization ya E-Card: kuongeza majina, tarehe, eneo, na maelezo mengine muhimu ya tukio.
Kila E-Card inapata QR code ya kipekee, ambayo itakuwa tayari kwa inspection siku ya tukio. Wageni wanaoweza kuonesha QR code hii wanapofika kwenye tukio.
Mteja anatupa orodha ya mawasiliano ya wageni wake. Hii inatupa uwezo wa kutuma E-Card moja kwa moja kwa kila mgeni kupitia SMS au barua pepe (inaweza pia kuwa WhatsApp).
Wageni wanapokea E-Card zao kabla ya tukio au wakati wa tukio, wakiwa na taarifa zote muhimu na QR code yao. Hii inarahisisha kuhudhuriwa na uthibitisho wa wageni.
Baada ya tukio kumalizika, wageni wanapokea SMS za shukrani kutoka kwa mteja, zikithibitisha uwepo wao na kuonyesha thamani ya kushiriki kwao kwenye tukio hili.